16 Oktoba 2020

Mkuu wa Idara ya Mazingira awaasa watumishi, akiwaaga waliostaafu

Na: Hashim Jumbe

Mkuu wa Idara ya Hifadhi ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu Manispaa ya Ilala, Ndugu Abdon Mapunda, amewaasa watumishi wa idara yake kufanya kazi kwa weledi na kujituma ili kuweza kufikia malengo waliojiwekea kama idara.

Hayo ameyasema leo wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watumishi wanne waliostaafu utumishi wa umma katika idara hiyo.

"Kwanza niwapongeze kwa kulitumikia Taifa mpaka kufikia kustaafu utumishi wa umma, ni faraja na heshima kubwa mno mmeipata, lakini pia niendelee kuwaasa mnaoendelea na utumishi wa umma kujitoa na kuwa waadilifu katika kazi zenu ndipo mtaweza kufanikiwa" alisema bwana Mapunda.

Itakumbukwa kuwa, idara  ya hifadhi ya mazingira na udhibiti taka ngumu, imekuwa na utamaduni wa kila mwaka kukutana na kufanya tathmini ya kiutendaji pamoja na wadau wao wa mazingira, huku wakitumia nafasi hiyo kuwapongeza waliofanya vizuri.

Aidha, kwa mwaka huu kikao hicho kimeambatana na kuwaaga watumishi watano waliomaliza muda wao ambao ni; Feada Magesa, Abdallah Waziri, Selemani Omary, Edward Mwasumbwe na Emmanuel MagangaHakuna maoni:

Chapisha Maoni