28 Aprili 2020

Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii Manispaa ya Ilala yafanya ziara ya ukaguzi, huku ikichukua tahadhari ya Corona

Na: Hashim Jumbe
Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii Manispaa ya Ilala, leo tarehe 28 Aprili, 2020 imefanya ziara yake ya kawaida kukagua Miradi iliyotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kipindi cha Robo ya Tatu ya Januari-Machi, 2020, huku Wajumbe wa Kati hiyo wakichukua tahadhari ya ugonjwa wa Corona, kwa kuvaa Barakoa na tahadhari nyengine.

Aidha, Kamati hiyo inayosimamia Miradi katika Sekta za Afya, Elimu, Kilimo, Uvuvi na Ufugaji ilitembelea Shule mpya ya Sekondari ya Minazi Mirefu ambayo ujenzi wake unakaribia kukamilika, miradi mingine waliyotembelea ni Machinjio ya Kisasa ya Vingunguti, Ujenzi wa Vyumba Vinne vya Madarasa Shule ya Sekondari Mchanganyiko na Ujenzi wa Soko la Kisasa la Kisutu.

Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Abdulkarim S. Masamaki akiongea wakati wa majumuisho ya ziara hiyo alisema "Nimeridhishwa na hali ya Miradi inavyokwenda, na ninawaomba Halmashauri muendelee kuisimamia miradi hii ikamilike kwa wakati uliowekwa, na miradi ambayo imetolewa mapendekezo na Wajumbe, nayo muifanyie kazi" 

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii Manispaa ya Ilala, wakiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Abdulkarim S. Masamaki walipotembelea machinjio ya kisasa ya Vingunguti na kukagua ujenzi wa machinjio hayo.
Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii Manispaa ya Ilala, wakipatiwa maelekezo ya ujenzi wa mradi wa machinjio ya Vingunguti
Mkuu wa Shule ya Sekondari Mchanganyiko wa kwanza kushoto, akitoa maelezo ya ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii walipofanya ziara Shule hapo
Diwani wa Kata ya Gerezani Mhe. Fatuma A. Ally ni mmoja kati ya Wajumbe wa Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii Manispaa ya Ilala akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Manispaa ya Ilala kwa kipindi cha Robo ya Tatu (Januari-Machi,2020)
Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii Manispaa ya Ilala, ikipata maelezo ya vizimba vitakavyokuwa katika Soko la Kisasa la Kisutu
Kamati ilipotembelea Shule mpya ya Sekondari ya Minazi MirefuHakuna maoni:

Chapisha Maoni